19/01/2022
Jinsi Ya Kupima Uwezo Wako Wa Kutimiza Malengo Yako 2022
Umeshawahi kujifanyia “ECG test”?.
Hiki ni kipimo muhimu na rahisi sana kitakachokupa muelekeo wa kujua uwezo wako wa kutimiza MALENGO YAKO na kufanikiwa ama la.
Kipimo hiki kinaangalia mambo 3 Makubwa:
______
E - (Excuses) VISINGIZIO:
Mtu ambaye kila wakati anatoa visingizio kuhusiana na kushindwa kufanya jambo fulani.
Mtu huyu atatumia visingizio vya mazingira, watu kumkwamisha, kukosa pesa n.k.
Ukishindwa kuvuka kwenye kipimo hiki utachelewa kufanikiwa.
Watu waliovuka ni wale wanaosema...
..“BILA KUJALI KINACHONIZUIA, NITAFANYA KILICHOPO NDANI YA UWEZO WANGU KWA SASA, SITAACHA”.
______
C - (Complacency) KURIDHIKA:
Hii inamaanisha mtu ambaye ameshakubali MATOKEO na HAAMINI k**a kuna kitu anaweza KUFANYA tena kuhusiana na HALI yake.
Huyu utakuta anasema “MI NAONA MUNGU NDIO AMEPENDA NIWE HIVI, SINA TENA CHA KUFANYA”.
Wakati mwingine anaona k**a AMESHAFIKA tayari, kwa sababu akijilinganisha na WENGINE ANAJIONA YUKO JUU SANA.
______
G - (Goal) MALENGO:
Ukichunguza ukajiona hauna malengo yoyote yanayoeleweka kuhusiana na maisha yako, ujue umeshafeli kipimo.
Malengo sio matamanio uliyonayo KICHWANI...
..Inatakiwa uyaandike MAHALI.
Uweke na Mipango ya namna ya kuyakamilisha na kila siku uwe unafanya Kitu kuelekea MALENGO YAKO.
Je, wewe umeyaandika na unayafanyia kazi?
Je, ni kitu gani katika kipimo cha “ECG” ambacho wewe unakikosa?
Kujifunza zaidi nashauri usome kitabu changu cha "Timiza Malengo Yako"
Unaweza kukipata kwa Tsh 15,000 tu! kutoka kwa:
+255 762 312 171
+255 745 252 670
See You At The Top
Joel Arthur Nanauka