25/04/2026
Tujifunze Jambo Kupitia Mradi Wa AKM GLITTER Uliokusanya Vijana Kwaajili Ya Kujifunza Ufugaji Wa Kuku...
✍️Mradi Ulijukana Kwa Jina La TANGA YETU Kwasababu Huo Mradi Ulifanyikia MKOA WA TANGA...
🧲Wahenga Wanasema Ukistaajabu Ya Musa Utaona Ya Firauni Ndivyo Mambo Yanavyokwenda Hapa Duniani...
🧲🧲Mradi Ulikua Na Lengo Kuu Moja Kuwafundisha Vijana Buree Ili Wapate Ujuzi Wa Vitendo Namna Ya Kufuga Kuku Wakiamini Baada Ya Hayo Mafunzo Itawasaidia Kubadili Maisha Yao Kupitia Ufugaji Wa Kuku...
💥Mpango Kazi Ulipangwa Vizuri Kupitia Wataalam Mbalimbali Kwa Ufupi Mradi Ulikua Umejiandaa Vizuri Sana Kuliko Kawaida K**a Unavyoona Kwenye Picha Namna Ambavyo Mipango Ilivyopangika Vizuri...
💥💥Kikubwa Ninachotaka Kukujuza Ni Kwamba Mradi Ulikua Unahitaji Watu Wenye Kujitoa Kwamaana Hakuna Jambo Jepesi Kwenye Kufanikisha Kitu Chochote Duniani Ijapokua Utaandaliwa Kila Kitu Au Kupewa Kila Kitu...
🙄Kilichonishangaza Ni Kwamba Licha Ya Lengo Kuwa Zuri Ila Kuna Baadhi Ya Vijana Waliishia Njiani Yaani Hapo Ndipo Utaamini Mafanikio Sio Ya Kila Mtu...
🙄🙄Kumbuka Maandalizi Ya Mradi Ulifanywa Na Kampuni kuanzia UJENZI WA MABANDA,VIFAA VYA KUFUGIA,CHAKULA CHA KUKU,VIFARANGA,MADAWA NA HUDUMA ZOTE ZINAZOHITAJIKA KWENYE KUFANIKISHA ILO JAMBO YAANI HADI WATAALAM WALIKUWEPO KWENYE HUO MRADI...
🔥Hapo Ndipo Nikajifunza Kufanikiwa Inaanzia Moyoni Na Sio Kukurupuka Kwa Mihemko Naamini Kupitia Huo Mradi Wapo Walionufaika Na Kutumia Hayo Mafunzo K**a Sehemu Ya Kutengeneza Ajira Binafsi Ila Pia Wale Ambao Waliishia Njiani Naona Ufugaji Haukua Sehemu Ya Ndoto Zao Ila Waliingia Tu Kwasababu Ya Hamasa Ya Hayo Mafunzo...
🔥🔥Nenda YOU TUBE Andika TANGA YETU Utajifunza Namna Ambavyo Watu Wanaandaa Mradi Hadi Kufikia Malengo Husika Binafsi Hayo Mafunzo Niliyafatilia K**a Sehemu Ya Kunijenga Kimaarifa Na Wewe Unaweza Nufaika Pia...
NB;Nakala Hii Haipo Kwaajili Ya Kupromote Huo Mradi Maana Umefanyika Miaka 3 Iliyopita Lengo Langu Ni Ujifunze Kuwa Kufanikiwa Ni Moyo Na Sio Mihemko...