02/10/2026
Umuhimu wa ukubwa wa punje za chakula
Kwenye chakula cha kuku ingredients zinazotumika kwa sehemu kubwa ni mahindi na soya
Ingredients nyingine ni mashudu ya alizeti, pumba za mahindi etc
Kwasababu kuku Hana meno k**a binadamu inabidi hizo ingredients zivunjwe vunjwe au kusagwa ili kuku aweze kula
Ukiwapa kuku wako chakula Bora lakini kina punje kubwa Bado hutapata matokeo unayotarajia
Hivyo basi kwa formula yetu ya vifaranga ni muhimu kuzingatia haya :
1.Mahindi yaparazwe kwa kutumia chekeche la vifaranga, kwenye mashine za chakula wanaelewa hiyo lugha lengo ni kupata saizi ya mahindi yanayoweza kuliwa na vifaranga
2.Soya kavu inatumika k**a ilivyo, na hapa tunatumia soya kavu na soya mafuta...soya kavuusiisage maana itakuwa na vumbi sana hii itakuletea mafua ila k**a soya uliyopata ina saizi kubwa iparaze - hasa kwenye formula tunayotumia soya mafuta[FFS] soya mafuta huwa ina mabonge mabonge
3.Mashudu ya alizeti yasagwe, zingatia kwenye formula ya vifaranga yanatumika kiasi kidogo
4.Mafuta/ Oil yanatumika kuongeza energy kwenye chakula, kupunguza vumbi na kuweka ladha
Nimewahi kufanya majaribio ya chakula chenye mafuta na kisicho na mafuta kwa kuondoa mafuta kwenye formula kwa kuku wa broiler
Chakula chenye mafuta ulaji uliongezeka kulinganisha na chakula kisicho na mafuta
Pia mafuta yanatumika kidogo, tunatumia kilo 2 kwenye kilo 100
Ndio kilo sio Lita, tunatumia kipimo Cha aina moja kwa ingredients zote ziwe za kimiminika au unga k**a unataka kutumia kipimo cha lita utaweka Lita 2.26 ambazo ni sawa na kilo 2
Mafuta yanawekwa mwishoni kabisa ukishachanganya ingredients zote zikachanganyika vizuri, unaweza kutumia mafuta ya alizeti,soya etc kiujumla ni mafuta ya mboga/kupikia
5.CFP ya vifaranga inatumika kilo 5 kwenye chakula kilo 100 au kilo 25 kwenye chakula kilo 500, CFP ya vifaranga inatumika kuchanganya chakula kuanzia siku 1
Mwisho, ni muhimu kuzingatia haya mambo hapo juu ili uweze kufikia malengo yako 🙏🏿
Tuna CFP ya vifaranga, kuku wanaokua na Wanaotaga
Bei za CFP hapa Dodoma
1.Starter/vifaranga [kuanzia siku 1 na kuendelea]
Kilo 5 ni 18,000
Kilo 25 ni 80,000
2.Grower/kuku wanaokua [Kuanzia siku 25 na kuendelea]
Kilo 5 ni 15,000
Kilo 25 ni 65,000
3.Kuku wanaotaga[Baada ya kuona yai]
Kilo 5 ni 15,000
Kilo 25 ni 65,000
𝐊𝐢𝐥𝐨 𝟓 𝐢𝐧𝐚𝐭𝐨𝐬𝐡𝐚 𝐤𝐮𝐜𝐡𝐚𝐧𝐠𝐚𝐧𝐲𝐚 𝐜𝐡𝐚𝐤𝐮𝐥𝐚 𝐤𝐢𝐥𝐨 𝟏𝟎𝟎
𝐊𝐢𝐥𝐨 𝟐𝟓 𝐢𝐧𝐚𝐭𝐨𝐬𝐡𝐚 𝐤𝐮𝐜𝐡𝐚𝐧𝐠𝐚𝐧𝐲𝐚 𝐜𝐡𝐚𝐤𝐮𝐥𝐚 𝐤𝐢𝐥𝐨 𝟓𝟎𝟎
Mawasiliano 0752912132
Moshi Agrovet tunapatikana Dodoma Majengo Sokoni