Ashton Frost One

Ashton Frost One Politics Sports and entertainment

14/08/2026

Wakili Peter Madeleka awasha moto kwa polisi kuita watu wahalifu kabla hawajatuhumiwa

Kapteni wa Yanga sc Bakari Nondo Mwamnyeto amewaalika wananchi kuelekea mechi ya kesho dhidi ya Namungo FC mechi ya ufun...
14/08/2026

Kapteni wa Yanga sc Bakari Nondo Mwamnyeto amewaalika wananchi kuelekea mechi ya kesho dhidi ya Namungo FC mechi ya ufunguzi wa ligi kuu

Kapteni amesema kesho tunaenda kuchukua point tatu kwa namungo wananchi wajitokeze kwa wingi kila mechi kwetu k**a fainali

14/08/2026

Sikiliza maneno ya lissu hapo

Kesi ya uhaini ya mh Tundu Antipas Lissu imeahirishwa leo kutokana na hali ya shahidi wa 18 kuumwa , upande wa jamuhuri ...
14/08/2026

Kesi ya uhaini ya mh Tundu Antipas Lissu imeahirishwa leo kutokana na hali ya shahidi wa 18 kuumwa , upande wa jamuhuri wanasema sisi sote ni binadamu tunapitia changamoto hivyo shahidi wetu leo ameugua yuko Muhimbili anahudhuris clinic

Mh lissu amekataa ombi hilo kwa kusema k**a mmekata pumzi fungeni mashahidi

Upande wa majaji wamekubaliana kesi kuendelea jumatatu kuwaonya upande wa jamuhuri kuleta mashahidi wote waliobaki ambapo bado mashahidi 12

Unafungua kesi alafu wewe ndo unalazimishwa ulete mashahidi sasa umefungua ya nini hii jamuhuri au takataka  Leo Agosti ...
14/08/2026

Unafungua kesi alafu wewe ndo unalazimishwa ulete mashahidi sasa umefungua ya nini hii jamuhuri au takataka



Leo Agosti 14, 2026

Jana tuliishia part 242 so leo tunaendelea na -;

Part 243

Imepigwa high Court ila tofauti na siku nyingine leo kaipiga Mwakasala

Majaji wameingia,

Karani wa Mahak**a anasimama kusoma namba ya shauri.

Mawakili wa Serikali wamekaa k**a hawana shahidi leo maana hawaeleweki.

Crimina 19605/2025 Jamhuri dhidi ya Lissu. kisha karani anakaa chini.

Iwapendeze naitwa Ajuaye, Ignas mwinuka, Thawabu Issa, Cattbert Mbilinyi na Winniwa Kasawa na Msh*takiwa yupo kizimbani.

Na shauri limekuja kwa ajili ya kusikilizwa.

Waheshimiwa Majaji shahidi tuliyemuandaa leo amepata dharula kwahiyo ameenda muhimbili kwahiyo tunaomba ahirisho hadi jumatatu tutaleta mashahidi wetu wote.

Mheshimiwa Tundu Lissu anacheka tu. Kile kicheko cha kusema hivi haya majitu yana akili kweli? Unakijua kile kicheko cha hasira na cha kusema wewe ni mpumbavu nini?

Watu wanasonya sana.

Majaji wanaandika kidogo hapa.

Ngoja tusubiri Mheshimiwa Lissu anasemaje.

Amesimama anasema mimi niko tayari kuendelea na kesi le, ninapinga ombi la kuahirisha kesi hii kutokana na sababu zilizotolewa na wakili wa serikali.

Kulikuwa na amri ambayo mlitoa mwaka jana kwamba upande wa Mash*taka ulete mashahidi wasiopungua wawili kila siku kesi hii inaposikilizwa. Na hii amri mmeirudia juzi ukiachia jana, siku ya Jumatano na mmeirudia jana.

Upande wa mash*taka walete mashahidi wengi sasa hautekelezi amri za Mahak**a kwasababu wanaamini nyie Majaji mmeshindwa kuwachukulia hatua na wanajua Mahak**a itawakubalia.

Mimi kusema maneno haya sio kitu chepesi sana lakini naamini hamjachukua hatua kabisa. Kila siku mnawapa maelekezo wao wanapuuza. Wanatuaminisha hapa na Dunia kuwa wanaweza kufanya lolote.

Sasa kwa vile jana mlirudia tena kwamba walete mashahidi na hawajaleta.

Msikubali Mahak**a kuu ya Tanzania ikageuzwa k**a ile Mahak**a iliyomuhukumu Jomo Kenyatta. Mahak**a ya Jaji Thucker ilisemwa kule London kuwa iliwakubalia kila kitu kilichoombwa na Mawakili wa serikali.

Msije mkafanywa hivyo, msiwakubalie mambo yasiyokuwa na msingi kwanini hawako tayari kuheshimu maamuzi ya Mahak**a.???

Mimi naamini wamekata pumzi na huyu mbaya wao aendelee kusota gerezani na wao waendelee kuvuta posho za Serikali, Msikubali kugeuzwa k**a hiyo mahak**a niliyoisema.

Again for the record hii ndio kesi kubwa kuliko zote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo hii mahak**a inapaswa kuonekana ikisimamia amri zake ili kulinda hadhi ya Mahak**a.

Hatutembelei kwenye njia ambayo haijafagilia. 1970, Grey Likungu Mataka kesi ya ugaidi ya kwanza.

Kesi ilichukua miezi sita kuanzia Mahak**a kuu hadi ile ya rufani, njia hii ikasafishwa vizuri zaidi Mwaka 1982 Khatibu Gandi na wenzake katika Mahak**a Kuu chumba hiki hiki kesi ilichukua mwaka 1 na siku 17.

Na haya ninayosema yapo kwenye record ya hizo kesi mbili kwahiyo mnayo mifano. Leo ni siku ya 493 yani mwaka 1 na miezi 4 hatujamaliza.

Nikija kusema aitwe Samia Suluhu Hassan si itachukua miaka 5 mtastaafu bila kesi hii kuitwa.

Maana nataka Philip Mpango, Kassim Majali na IGP nikisema waje kesi si haitaitwa milele? Jitahidini hii Mahak**a isiwe Kangaroo Court.

Nimemaliza.

Anasimama Ajuaye, Wakili wa Serikali tumemsikia mwenzetu alichoongea lakini mashahidi ni wanadamu na kwakuwa wanadamu changamoto inaweza kutokea muda wowote na kwa binadamu yeyote.

Sisi upande wa mash*taka tunakili kuwa ni kweli bado tuna mashahidi wengi lakini sio lazima tulete wote, pengine ni shahidi wa mwisho na ndio huyo tunayemtegemea sasa hakuna namna kifungu cha 265 CPA.

Tunaomba Mahak**a yenu iahirishe shauri hili mpaka Jumatatu na tutaleta mashahidi wote waliobakia, wote kabisa waliobakia na itakuwa ndani ya session hii na kikao hiki kilichopangwa.

Part 244 itaendelea kwenye post inayofuata.

Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt Dorothy Gwajim...
13/08/2026

Kupitia ukurasa wa Instagram wa waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt Dorothy Gwajima ameandika ujumbe huu:

Mnanitag sana kuhusu hawa kwenye picha. Bahati mbaya niko sehemu siwezi kuwasha sauti ila, kwa sms mnazotuma nimeona niwajulishe kuwa nimepokea nami niwashauri mtag .tanzania Mhe Waziri wa Mambo ya ndani ili wafahamu waone hatua za kuchukua kulingana na hali halisi ilivyo.

Nabii tito amekuwa akitoa tamko na vitisho vya mara kwa mara kuhusu Rais samia n.k

Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Dkt. Charles Kitima, amesisitiza kuwa mkwamo wa kisiasa...
13/08/2026

Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Dkt. Charles Kitima, amesisitiza kuwa mkwamo wa kisiasa nchini utatatuliwa tu ikiwa kutakuwa na utayari wa kukiri makosa, kusimamia ukweli, na kuombana msamaha kufuatia matukio yaliyogubika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 13, 2026, kufuatia mkutano kati ya TEC na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan uliofanyika Ikulu ya Chamwino tarehe 10 Agosti, Padre Kitima amebainisha kuwa msingi wa andiko walilomkabidhi Rais ni kuhakikisha nchi inapata uponyaji wa kweli.

Padre Kitima ameeleza kuwa viongozi wa kiroho wanaona kuna haja ya kuwa na ujasiri wa kutaja kile kilichokwenda mrama ili kurejesha mahusiano yaliyovunjika kati ya serikali na wananchi. Amebainisha kuwa bila kukiri ukweli wa yaliyotokea, mchakato wa maridhiano hautakuwa na tija

“Kutokana pia na kwamba waliweka bayana kwamba ili tutoke katika hali hii inabidi kwenda katika kusimamia ukweli na vile vile kutakana msamaha kusameheana na hata kuponya nchi. Kwa hiyo kwa kiingereza tunasema ‘to admit the truth then reconciliation healing the nation’,” amesisitiza Padre Kitima

Katibu Mkuu huyo amekiri kuwa matukio ya tarehe 29 Oktoba 2025 yameacha sononeko kubwa kwa Watanzania wengi na kuharibu imani ya raia kwa mamlaka zao. Amesisitiza kuwa maaskofu wameweka wazi masikitiko yao kuhusu mauaji na uharibifu wa mali uliotokea na kwamba sasa ni wakati wa kutatua mambo hayo yaliyosababisha watu kuingia katika hali ya maandamano

TATIZO UWAZI WA MATUMIZI Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis M***a Omar (Mb), ameimwagia sifa Mamlaka ya Mapato Tanzania...
13/08/2026

TATIZO UWAZI WA MATUMIZI

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis M***a Omar (Mb), ameimwagia sifa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kuendelea kuvuka malengo ya ukusanyaji wa mapato kila mwezi, akieleza imani yake kuwa kwa kushirikiana na walipakodi, wataweza kuvuka lengo la kukusanya zaidi ya shilingi trilioni 42 katika Mwaka wa Fedha 2026/2027.

Sifa hizo zinafuatia maelezo ya Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Yusuph Mwenda, kuwa katika mwezi Julai 2026, TRA ilikusanya zaidi ya shilingi trilioni 3.245 ikilinganishwa na lengo la shilingi trilioni 2.971, sawa na ufanisi wa asilimia 109 ya lengo na ukuaji wa asilimia 21.

Aidha, CPA Mwenda amesema katika kipindi hicho TRA imefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 325, fedha ambazo ni asilimia 70 ya makusanyo yote na kuzipeleka moja kwa moja kwenye Mifuko 11 ya ujenzi wa miundombinu katika sekta mbalimbali zikiwemo barabara, maji na utalii.

Wakili na mwanasheria wa Mahak**a kuu ya Tanzania Peter madeleka ameamua kuish*taki mahak**a kwa kuvunja sheria kufuatia...
13/08/2026

Wakili na mwanasheria wa Mahak**a kuu ya Tanzania Peter madeleka ameamua kuish*taki mahak**a kwa kuvunja sheria kufuatia katazo la wanasheria kuongea na vyombo vya habari kila mara watokapo mahak**ani

Wakili peter madeleka amesema haya kupitia mtandao wa X
"Nitafungua KESI YA KIKATIBA dhidi ya MAHAKAMA KUU YA TANZANIA kupinga KATAZO hilo 👇, ambalo LIVUNJA ibara ya 18(b) ya KATIBA ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania."

13/08/2026

WANANCHI MATEJO WAMLILIA KIJANA ALIYEFARIKI BAADA YA KUKUTANA NA ASKARI NGORONGORO

Wananchi wa Mtaa wa Matejo, Kata ya Sakina jijini Arusha, wameeleza masikitiko yao kufuatia kifo cha kijana aliyefariki dunia jana baada ya kudaiwa kukumbwa na tukio akiwa safarini kuelekea Magugu kwa ajili ya msiba.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na wananchi, kijana huyo alikuwa pamoja na wenzake wawili wakielekea Magugu, lakini walipotea njia na baadaye kuelekea upande wa Ngorongoro.

Walipofika eneo hilo, inadaiwa walikutana na askari wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, ambao waliwak**ata na kuwapa adhabu.

Wananchi wanadai kuwa baada ya tukio hilo, hali ya kijana huyo ilibadilika na hatimaye alifariki dunia.

Timu yetu imefika msibani Matejo na kuzungumza na wananchi pamoja na ndugu wa marehemu, ambao wameeleza kwa uchungu walichokiona na wanachokifahamu kuhusu tukio hilo.

Wananchi wameitaka mamlaka husika kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini kilichosababisha kifo cha kijana huyo na kuhakikisha ukweli wa tukio hilo unafahamika.

Address

Dar Es Salaam

Telephone

+255764020265

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ashton Frost One posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Ashton Frost One:

Shortcuts

Share