30/09/2026
WAITWAO NI WENGI
(Mathayo 22:14)
[14] Kwa maana waitwao ni wengi, bali wateule ni "wachache".
Hakika, Tuneitwa
wengi ndiyo, ila 'wateule' ni 'wachache':
Kwa sababu hiyo, huu si wakati Sahihi wa "Kurushiana Mawe", kwa vile 'tumeitwa zote'!
Swala la mtu kuwa 'Mteule', hilo ni la Mzee wa Siku mwenyewe, Maana ndiye aliyetuita zote, tena kwa Nyakati tofauti tofauti Shambani mwake.
Sasa basi, Ndugu na Dada Katika Mwili wa Kristo, Amani iwe kwanu Katika hili la Mtumishi wa Mungu "Joel Lwaga";
(1Yohana 1:9)
[9] K**a tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni Mwaminifu na wa Haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.
Nataka tujue, kwa kuwa Neema inayookoa ingalipo, Mtu ye yote, tena toka Dhehebu Lolote, Akiweza Kuungama dhambi, Akatubu kwa Kumaanisha Kuziacha Kabisa Kabisa!
Huyu Mungu aliye Mwaminifu na wa Haki Aweza Kumwondolea dhambi zote, na kuziweka mbali naye hata akawa Mtakatifu, maana Mlango wa Wokovu bado upo wazi kwa kila Aaminiye.
INENAVYO BIBLIA
(2Wakorintho 6:14-18)
[14] Msifungiwe Nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana rafiki gani kati ya "Haki na Uasi"? Tena pana 'Shirika' gani kati ya "Nuru na Giza"?
[15] Tena pana ulinganifu gani ya "Kristo na Beliari"? Au yeye 'Aaminiye' ana sehemu gani pamoja na yeye 'asiyeamini'?
[16] Tena pana 'mapatano' gani kati ya "Hekalu la Mungu" na 'Sanamu'? Kwa maana sisi tu Hekalu la Mungu aliye Hai; k**a Mungu alivyosema, ya kwamba. 'Nitakaa ndani' yao, na kati yao 'Nitatembea', nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
[17] Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema ADONAY, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami 'nitawakaribisha'.
[18] Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa k**e, asema ADONAY Mwenyezi.
â—‡ Jambo la kwanza, Bila shaka Mpaka hapa tulipofika, Nadhani Mtumishi wa Mungu "Joel Lwaga" 'Umefungiwa' NIRA Pamoja na mtu 'asiyeamini', kwa jinsi isivyo Sawasawa;
Haikosi, hapa ndipo Chanzo cha Mzozo wote huu unaoendelea katika vyombo vya Kijamii.
â—‡ Jambo la Pili, "Joel Lwaga", Wewe ni "Hekalu la Mungu", ni Nyumba yake IBADA ya "Kusifu na Kuabudu", Lakini pia, Mungu Anakaa ndani yako.
â—‡ Jambo la tatu, Yeye Anasema, Toka kati yake Ukatengwe naye, ili Mungu Awe Baba kwako.
Ndugu yangu, Mdogo wangu katika Mwili wa Kristo, "Joel Lwaga" Una Uhuru "Kufanya Machaguo" Sahihi katika maisha na Usiingiliwe na mtu awaye yote!
Lakini, Kumbuka wewe ni 'Mti Matunda' ya "Makatapela", Ndugu zako katika mwili wa Kristo Wameshaonja 'Utamu wa Matunda' yatokayo kwenye 'Mti wewe';
Hakika, Hawataki kabisa Kukosa Matunda hayo, Ndiyo maana Kelele zimekuwa nyingi Mno mnomno..!!
Sasa, K**a Nilivyotangulia kusema, niseme tena, Una Uhuru "Kufanya Machaguo" Sahihi na mambo mengine yaendelea kwa Utukufu wake Mzee wa Siku.
Bila shaka, wewe ni mtu Mzima kimwili na kiroho, Tumia Utu Uzima wako kufanya haya yafuatayo;
▪︎ 'Tizama' kwa Makini Sana, ili Uone kwa Usahihi sana!
▪︎ 'Angalia" kwa Kina, kisha,
▪︎ Upate 'Kuona" Kitu kile 'Unachotaka' Kuona Kupitia "Kipawa" chako cha Uimbaji.
1) K**a Ufalme na Haki yake, ili hayo mengine Uzidishiwe kwa wakati wake..
2) K**a Mali za Ulimwengu huu, Upate kwa viwango vya juu Sana kupita matarajio ya wengi.
{Hata hivyo, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa}
Imenenwa:
Kipawa cha Mtu Humtajirisha yeye aliyenacho, Nami Nadhani, Kutajirishwa na Kipawa chako ni Ndoto ya kila mwenye Kipawa chake.
Hata hivyo, aliyepewa Vingi, kwake huyo watataka vingi.
Hebu Tuombe Pamoja!
[Sikiza, Ee ISRAEL; ADONAY, ELOHEINU wetu, ADONAY Ndiye Mmoja.
Nawe Mpende ADONAY, ELOHEINU wako, Kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa Nguvu zako zote.]
(Kumbu/ la Torati 6:4-6)
{Ee ADONAY ELOHEINU wetu, Kwa Jina Lile Lipitalo Majina yote, YESHUAH HAMASHIACH (Yesu Kristo) Namwinua Mtumishi wako "Joel Lwaga" katika Majira haya ya Kurushiwa Mawe kila Upande!}
[Hata hivyo, wewe unawajua walio wako, Joel Lwaga ni wako Ee ADONAY, tena wewe Ndiye Ukiyemwita kwa Jina lake, na Ukampa Kipawa Cha Kukusifu, Kukuabudu, Kuwatia Moyo watu wako kwa njia ya Nyimbo zake;]
{Sasa, Katika Jina la Yesu Kristo wa Nazareth, Mwana wa Mungu aliye Hai, Aomba Umsimamishe kwenye Njia iliyo Sahihi na Kunyoka, Mtie Nguvu za kiroho katika roho yake ili Apate Kuona Mahali Sahihi kwa wakati Sahihi!}
[Ulimwokoa Mwenyewe Hakika Hutamwacha Apotee, Kwa kuwa Neno lako inasema; Ajaye kwako, Hutamtupa Nje kamwe.
Ni kwa Jina la Yesu Kristo wa Nazareth, Nimeomba na Kuamini, Amina tena Amina.]